1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yadungua droni mbili za Ukraine karibu na Moscow

9 Agosti 2023

Urusi imesema imezidungua ndege mbili za Ukraine zisizoruka na rubani karibu na Moscow. Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema droni moja iliangushwa kusini mwa mji huo na nyingine upande wa Magharibi.

https://p.dw.com/p/4Uwre
Moskau Drohnenangriff auf Hochhaus
Picha: EVGENIA NOVOZHENINA/REUTERS

Mashambulizi ya angani yanayofanywa na ndege zisizoruka na rubani ndani ya Urusi yameongezeka tangu droni ilipoharibiwa karibu na Ikulu ya Kremlin mapema Mei.

Maeneo ya kiraia ya mji huo mkuu yalipigwa baadae mwezi Mei na eneo la kibiashara la Moscow likalengwa mara mbili katika siku tatu mapema mwezi huu.

Ukraine huwa haitoi kauli yoyote kuhusiana na nani anayehusika na mashambulizi hayo kwenye mipaka ya Urusi, isipokuwa maafisa wameelezea hadharani kuridhishwa nayo.