1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yamtia nguvuni jasusi wa kike wa Urusi

8 Agosti 2023

Shirika la ujasusi wa ndani la Ukraine, SBU, limemtia nguvuni mwanamke mmoja anayetuhumiwa kukusanya taarifa za safari za Rais Volodymyr Zelensky na pia kujaribu kuitumia Urusi taarifa za kijeshi.

https://p.dw.com/p/4UtGT
Ukraine
Maafisa wa idara ya usalama ya UkrainePicha: Felipe Dana/AP Photo/picture alliance

Shirika la ujasusi wa ndani la Ukraine, SBU, limemtia nguvuni mwanamke mmoja anayetuhumiwa kukusanya taarifa za safari za Rais Volodymyr Zelensky na pia kujaribu kuitumia Urusi taarifa za kijeshi.

Mshukiwa huyo ambaye hakutajwa jina wala kuoneshwa picha yake kwa uwazi, alikamatwa kwenye mji wa bandari wa Mykolaiv kusini mwa Ukraine, ambako Zelensky alitembelea tarehe 27 mwezi uliopita.

Soma zaidi kuhusu: Mzozo wa Ukraine

Shirika la SBU linamtuhumu pia jasusi huyo kwa kujaribu kuyatambuwa maeneo iliko mifumo ya kieletroniki ya kijeshi katika mji mwengine wa Ochakiv, ulio umbali wa maili 30 kutoka Mykolaiv. SBU imedai kumkamata mwanamke huyo akiwa anajaribu kutuma taarifa za kijasusi kwa jeshi la Urusi.

Mwanamke huyo alikuwa akifanya kazi kwenye duka la vifaa vya kijeshi. Tayari mahakama imesharidhia kukamatwa kwake, na endapo atapatikana na hatia atakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 12 jela.