1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yadai kutwaa mji muhimu magharibi ya Ukraine

4 Julai 2024

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema vikosi vyake vimetwaa udhibiti wa wilaya moja kwenye mji muhimu wa Ukraine, ingawa Kiev inasema eneo hilo bado limo kwenye mapigano makali.

https://p.dw.com/p/4hqJI

Mji wa Chasiv Yar upo umbali wa kilomita 20 kuelekea magharibi mwa mji wa Bakhmut, ambao ulitwaliwa na vikosi vya Urusi mwaka uliopita.

Soma zaidi: Mashambulizi ya Urusi yasababisha vifo vya watu 3 Dnipro

Pande zote mbili zinauchukulia mji wa Chasiv Yar kama eneo la kimkakati ambalo linaweza kutumiwa na Urusi kama sehemu ya kuanzisha mashambulizi kuelekea upande wa magharibi mwa Ukraine kupitia mkoa wa Donetsk kuelekea miji ya Kramatorsk na Sloviansk.

Afisa habari wa Kikosi cha 24 cha Ukraine, Ivan Petrechak, amesema hali ni ngumu ingawa kikosi chake bado kipo kwenye eneo hilo.