1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Mashambulizi ya Urusi yasababisha vifo vya watu 3 Dnipro

3 Julai 2024

Ndege ya Urusi isiyokuwa na rubani na msururu wa makombora ya angani katika mji wa kati wa Ukraine wa Dnipro yamesababisha vifo vya watu watatu na kuwajeruhi wengine zaidi ya dazeni moja.

https://p.dw.com/p/4hoqo
Ukraine | russischer Angriff auf Dnipro
Athari ya shambulio la Urusi mjini DniproPicha: facebook.com/zelenskyy.official/posts

Haya yamesemwa na gavana wa mkoa huo Sergiy Lysak.

Hali hii inatokea wakati ambapo mtu mwingine mmoja ameuwawa na wengine 4 kujeruhiwa kufuatia mashambulizi ya Urusi katika eneo la kaskazini mashariki la Kharkiv.

Soma pia: Urusi yailenga miundombinu ya nishati nchini Ukraine

Katika kijiji cha Ruska Lozova, watu wawili wamejeruhiwa na nyumba 10 kuharibiwa katika shambulizi lililofanywa alfajiri ya leo.

Urusi mara kwa mara imekuwa ikikanusha kuwalenga raia tangu ianzishe uvamizi wake wa Ukraine mnamo Februari mwaka 2022.