1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi na Ukraine zaendelea kushambuliana kwa kutumia droni

23 Agosti 2023

Urusi na Ukraine zimeshambuliana kwa kutumia droni mapema leo, huku Kyiv ikiripotiwa kuilenga Moscow kwa mara nyingine tena.

https://p.dw.com/p/4VTcu
Moscow
Sehemu ya jengo lililoharibiwa na droniPicha: picture alliance/AP

Urusi na Ukraine zimeshambuliana kwa kutumia droni mapema leo, huku Kyiv ikiripotiwa kuilenga Moscow kwa mara nyingine tena. Navyo vikosi vya Urusi vimefanya mashambulizi mengine kwenye maghala ya nafaka za Ukraine.Zelenskiy aamuru watu waondoke Donetsk

Mkuu wa Utawala wa Kijeshi wa mkoa wa Odesa Oleh Kiper amesema shambulizi la droni jana usiku katika mkoa wa kusini mwa Ukraine wa Odesa lilisababisha moto mkubwa katika maghala ya nafaka. Amesema mifumo ya ulinzi wa angani ya Ukraine ilizidungua droni tisa.

Wakati huo huo, maafisa wa Urusi wamedai kuzidungua droni za Ukraine mjini Moscow na eneo jirani mapema leo. Urusi yasema shambulizi la droni Kremlin lazima lilipizwe

Wizara ya Ulinzi na Meya wa Moscow wamesema hakuna hasara iliyoripotiwa katika shambulizi hilo la droni ambalo limekuwa kama tukio la kila siku katika mji huo mkuu wa Urusi.