1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi: Uingereza kupeleka kikosi Ukraine ni kutangaza vita

12 Januari 2024

Rais wa zamani wa Urusi, Dmitry Medvedev amesema hatua ya kupelekwa kwa kikosi chochote cha kijeshi cha Uingereza nchini Ukraine, itakuwa tangazo la vita dhidi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4bBFb
Moscow, Urusi | Rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi Dmitry MedvedevPicha: Yekaterina Shtukina/ITAR-TASS/IMAGO

Medvedev ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi ametoa matamshi hayo akijibu ziara ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak nchini Ukraine, ambapo ametangaza kuongeza ufadhili wa kijeshi kwa kuisaidia Ukraine kununua ndege mpya za kijeshi.

Medvedev ameandika leo katika mtandao wa kijamii wa Telegram kwamba ana matumaini maadui zao, Uingereza aliyosema imejaa "majivuno" inaelewa kuwa kupeleka kikosi rasmi cha kijeshi nchini Ukraine itakuwa tangazo la vita dhidi ya Urusi.

Soma pia:Zelenskiy asema usitishaji mapigano Ukraine utainufaisha tu Urusi

Pia ameyauliza mataifa ya Magharibi yatajisikia vipi iwapo ujumbe wa Sunak utashambuliwa katikati ya Kiev, jambo ambalo amesema limetokea hivi karibuni kwa raia wa Urusi kwenye mji wa Belgorod.