1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi kujadili hatma ya askari wake Nagorno-Karabakh

11 Oktoba 2023

Urusi leo imesema itajadili na Azerbaijan mustakabali wa walinda amani wake huko Nagorno-Karabakh, wiki chache baada ya Baku kuliteka tena eneo hilo lililojitenga ambalo lilikuwa linaendeshwa na Waarmenia.

https://p.dw.com/p/4XOSc
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Grigory Sysoyev/AFP

Hatua ya Urusi kutoingilia kati uvamizi wa haraka wa Azerbaijan, umeipelekea Armenia ihisi kutoungwa mkono na rafiki yake Moscow.

Sehemu kubwa ya Waarmenia 120,000waliokuwa Nagorno-Karabakhkwa sasa wamekimbilia Armenia.

Soma pia:Azerbaijan yamkamata rais wa zamani wa Nagorno-Karabakh

Azerbaijan ililiteka tena eneo hilo kufuatia zuio la miezi tisa la usambazaji chakula na nishati kuingia Nagorno-Karabakh na walinda amani wa Urusihawakuchukua hatua yoyote ile kufanya hali kuwa bora.