1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAzerbaijan

Azerbaijan yasema iko tayari kwa mazungumzo na Armenia

9 Oktoba 2023

Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, amesema jana Jumapili kwamba nchi yake iko tayari kufanya mazungumzo na Armenia kuhusu mkataba wa amani baada ya kulitwaa tena jimbo la Nagorno Karabakh lenye idadi kubwa ya Waarmenia

https://p.dw.com/p/4XH4g
Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev akizungumza katika kongamano la kimataifa mjini Baku mnamo Oktoba 2, 2023
Rais wa Azerbaijan Ilham AliyevPicha: Azerbaijani Presidency/AA/picture alliance

Rais Aliyev, alisema hayo alipofanya ziara Georgia baada ya kususia mkutano uliopangwa na waziri mkuu wa Armenia Nikol pashinyan pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya mjini Granada nchini Uhispania mnamo siku ya Alhamisi ambao Umoja wa Ulaya ulijaribu kusimamia.

Azerbaijan yaishkuru Georgia kwa msaada wake

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo ya jana mjini Tbilisi na waziri mkuu wa Georgia

Irakli Garibashvili, Aliyev alisema anaishukuru nchi hiyo kwa juhudi zake za upatanishi, na kuongeza kuwa Azerbaijan itakuwa

tayari kuhudhuria mazungumzo ya kujadili masuala yanayohusiana na mkataba wa amani ikiwa Armenia itakubali.