1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi kuangazia mapendekezo ya Afrika ya kuumaliza mzozo

28 Julai 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin leo amesema Moscow "inachunguza kwa makini" mapendekezo yaliyotolewa na baadhi ya viongozi wa Afrika yanayolenga kumaliza mzozo nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4UWIa
2nd Russia-Africa Summit: plenary session
Picha: Mikhail Tereshchenko/TASS/dpa/picture alliance

Mnamo mwezi Juni, wajumbe wa Afrika walifanya ziara kwanza nchini Ukraine halafu baadaye wakaelekea Urusi ili kutoa upatanishi katika mzozo huo.

Mapendekezo ya viongozi hao wa Afrika yalijumuisha kupunguzwa kwa shughuli za kijeshi, dhamana ya usalama kwa pande zote na kutambua uhuru wa kila mmoja.

Mkutano wa kilele kati ya Urusi na viongozi wa Afrika unakuja baada ya Urusi kujiondoa katika makubaliano ya kuruhusu usafirishaji wa nafaka kupitia Bahari Nyeusi, na kuzua wasiwasi miongoni mwa mataifa ya Afrika.