1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yadungua droni mbili za Ukraine huko Belgorod

11 Septemba 2023

Urusi imesema hii leo kuwa imedungua ndege mbili zisizo na rubani za Ukraine karibu na mpaka katika eneo la Belgorod. Hadi sasa hakuna majeruhi walioripotiwa.

https://p.dw.com/p/4WB4t
Ukraine I Kharkiv I Charkiw
Picha: Vadym Bielikov/AFP

Gavana wa mkoa wa Belgorod Vyacheslav Gladkov amesema droni hizo "zilidunguliwa" kwenye wilaya ya Yakovlevsky, iliyopo kaskazini magharibi mwa jiji la Belgorod. Usiku wa Alhamisi, ndege mbili zisizo na rubani za Ukraine zilidunguliwa huko Rostov-on-Don kusini-magharibi mwa Urusi.

Tangu Ukraine ilipoanzisha mashambulizi yake mapema mwezi Juni,  Urusi imestahimili wimbi la mashambulizi  ya ndege zisizo na rubani katika miezi ya hivi karibuni ambayo yameharibu mara kadhaa majengo nchini humo hasa katika mji mkuu Moscow.

Hayo yakijiri, Wafanyakazi wawili wa mashirika ya kutoa misaada, raia wa Canada na Uhispania, wameuawa karibu na Bakhmut, mashariki mwa Ukraine katika shambulio ambalo Kiev imesema limefanywa na Urusi jana Jumapili.