1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi kuwaondoa watoto katika vijiji vya mipakani

31 Mei 2023

Urusi imesema itawaondoa mamia ya watoto kwenye vijiji kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi kwenye mkoa wa Belgorod unaopakana na jimbo la Kharkiv, Ukraine.

https://p.dw.com/p/4S1YS
Picha ya kituo cha kuwatunza watoto waliotelekezwa na yatima katika mji wa St. Petersburg, Urusi. Urusi sasa inaangazia kuwahamisha watoto katika maeneo ya mipakani ili kuwaepusha na madhara ya vita.
Watoto wamekuwa miongoni mwa wahanga wakubwa wa mzozo kati ya Urusi na Ukraine. Picha: Shamukov Ruslan/ITAR-TASS/picture alliance

Gavana wa Belgorod Vyacheslav Gladkov, amesema kuanzia leo watawaondoa watoto kutoka kwenye wilaya za Shebekino na Graivoron, ambazo zimeathiriwa zaidi na mashambulizi yanayoongezeka ya Ukraine. Gladkov amesema hali inazidi kuwa mbaya katika kijiji cha Shebekino, ambacho asubuhi ya leo kilishambuliwa kwa kombora na kusababisha majeruhi wanne. Akizungumzia mashambulizi hayo, msemaji wa Ikulu ya Urusi, Kremlin Dmitry Peskov amesema hali inatisha. Jana mtu mmoja aliuawa na wengine wawili walijeruhiwa katika shambulizi la Ukraine katika kituo cha watu wasio na makaazi kwenye mkoa huo. Mashambulizi hayo yanafanyika wakati ambapo Ukraine inajiandaa kwa operesheni kubwa ya kijeshi dhidi ya vikosi vya Urusi.