1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaZimbabwe

Upinzani Zimbabwe taabani wakati wa chaguzi ndogo

9 Desemba 2023

Zimbabwe imeanza msururu wa uchaguzi mdogo huku upinzani ukiwa na msukosuko baada ya kuondolewa kwenye orodha ya sajili ya wapiga kura.

https://p.dw.com/p/4ZxtM
Chama kikuu cha upinzani Zimbabwe cha kumbwa na misukosuko
Chama kikuu cha upinzani Zimbabwe cha kumbwa na misukosukoPicha: Zinyange Auntony/AFP via Getty Images

Chaguzi tisa ndogo zilipaswa kufanyika lakini wagombea wengi wa upinzani waliondolewa kwenye orodha za uchaguzi na mahakama katika msururu wa machafuko kuelekea uchaguzi huo.

Tume ya uchaguzi ya Zimbabwe imesema kwenye mtandao wa X, kwamba vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa moja asubuhi, bila kutoa maelezo zaidi.

Wakazi wamesema hakuna upigaji kura uliofanyika katika wilaya ya Harare ambapo moja ya uchaguzi mdogo ulipangwa, kwa sababu mgombea wa chama tawala cha ZANU-PF alishinda bila kupingwa.

Badaa ya uchaguzi wa Agosti Rais Emmerson Mnangagwa alipata muhula wa pili, huku chama chake cha ZANU-PF kupata viti 177 kati ya 280 vya bunge na chama cha upinzani cha Citizens Coalition for Change kikichukua viti 104.

Lakini miezi miwili baadaye, wabunge 14 wa CCC walifukuzwa nje ya bunge na chaguzi ndogo tisa kuamriwa. Viti vingine vitano vinaamuliwa kwa uwakilishi sawa.