1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tembo wafa Mbuga ya Hwange Zimbabwe

8 Desemba 2023

Tembo kadhaa wamekufa kwa kiu katika mbuga maarufu ya wanyama ya Hwange nchini Zimbabwe.

https://p.dw.com/p/4ZwPE
Tembo wa Afrika.
Tembo wa Afrika.Picha: Tommy Mees/Pond5 Images/IMAGO Images

Wahifadhi wa mazingira na wanyamapori wanahofia kupoteza tembo zaidi kutokana na ukame uliosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na hali ya hewa ya El Nino ambayo inakausha vyanzo vya maji.

Afisa wa Mamlaka ya Mbuga na Wanyamapori ya Zimbabwe (Zimparks), Daphine Madhlamoto amesema mbuga ya Hwange haina mto mkubwa unaopita kati yake, na wanyama wanategemea visima vinavyotumia nishati ya jua.

Soma zaidi: Ukosefu wa maji walazimisha Tembo kuihama Zimbabwe

Idadi ya tembo katika mbuga ya Hwange ni 45,000 na tembo aliyepea anahitaji lita 200 za maji kila siku.

Lakini kutokana na vyanzo vya maji kupungua, pampu zinazotumia nishati ya jua kwenye visima 104, havijaweza kutoa maji ya kutosha. Madhlamoto amesema mbuga hiyo inashuhudia madhara ya mabadiliko ya tabia nchi, na wamekuwa wakipata mvua kidogo.