1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upande mmoja wa mzozo wa Sudan wasusia mazungumzo ya Geneva

12 Julai 2024

Pande zote zinazopigana nchini Sudan ziko mjini Geneva, Uswisi, kwa mazungumzo na mjumbe wa Umoja wa Mataifa, ingawa upande mmoja haukufika kwenye mkutano wa kwanza leo

https://p.dw.com/p/4iEl3
Andrew Gilmour msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa-haki za binadamu
Andrew Gilmour msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa-haki za binadamu akizungumza mjini Geneva kuhusu hali ya SudanPicha: SALVATORE DI NOLFI/Keystone/picture alliance

Pande zote zinazopigana nchini Sudan ziko mjini Geneva, Uswisi, kwa mazungumzo na mjumbe wa Umoja wa Mataifa, ingawa upande mmoja haukufika kwenye mkutano wa kwanza leo. Haya yamesemwa na msemaji wa Umoja wa Mataifa Alesandra Vellucci, bila kuweka wazi ni upande upi ambao haukuhudhuria.

Mazungumzo hayoyanafanyika kwa mfumo wa mjumbe binafsi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Ramtane Lamamra, kukutana na ujumbe wa kila upande katika vyumba tofauti. Wajumbe wa pande hizo mbili hawajapangiwa kukutanakwa mazungumzo ya ana kwa ana. Kulingana na msemaji wa Umoja wa Mataifa, Velluci, mazungumzo hayo yanafanyika kwa msingi wa maazimio mawili yaliyopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mapema mwaka huu. Maazimio hayo yanataka hatua zichukuliwe kuhakikisha usambazwaji wa misaada ya kiutu na kulindwa kwa raia kote nchini Sudan.