1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSudan

Jeshi laiteka maabara ya vijidudu vya magonjwa nchini Sudan

26 Aprili 2023

WHO imetahadharisha juu ya hatari inayoweza kuwakumba wakaazi wa mji mkuu wa Sudan, Khartoum kutokana na taarifa kwamba wanajeshi wa upande mmojawapo wameiteka maabara yenye vijidudu vinavyoweza kueneza magonjwa.

https://p.dw.com/p/4QZ2M
Sudan Khartum | Kämpfe zwischen Armee und RSF-Miliz | General Mohamed Hamdan Dagalo
Picha: MOHAMED NURELDIN ABDALLAH/REUTERS

Hata hivyo haijulikani ni upande gani wa jeshi ulioiteka maabara hiyo.

Kituo hicho kina bakteria wa maradhi ya kipindupindu na vijidudu vingine vya magonjwa ya hatari kubwa.

Mwakilishi wa asasi ya WHOamewaambia waandishi wa habari kwamba wataalamu hawajaweza kufika kwenye maabara hiyo ili kudhibiti usalama.

Mwakilishi huyo Nima Saeed Abid amesema wanajeshi waliwatimua wataalamu na kutwaa udhibiti wa maabara na kuigeuza kuwa kambi ya kijeshi.