1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

UN:Tunahitahi msaada mara mbili zaidi kwa wasudani

4 Septemba 2023

Umoja wa Mataifa umeongeza zaidi ya mara mbili kiwango cha msaada inaouhitaji kuwashughulikia takriban watu milioni mbili wanaotarajiwa kuikimbia Sudan inayokumbwa na vita, kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4Vwjd
Demokratische Republik Kongo | Binnenvertriebene im Flüchtlingslager Kanyaruchinya
Gari la UNHCR likishusha wakimbizi.Picha: Aubin Mukoni/AFP/Getty Images

Shirika la Umoja huo la kuhudumia wakimbizi,UNHCR na mashirika mengine  washirika wake,wametowa mwito wa kupatiwa dola bilioni 1 za kununua msaada wa mahitaji muhimu  pamoja na kuwalinda watu zaidi ya milioni 1.8 wanaotarajiwa kuwasili katika nchi jirani na Sudan kufikiwa mwishoni mwa mwaka huu.

Soma pia:Jenerali AbdelFatah al Burhani wa Sudan yupo ziarani Sudan

Awali shirika hilo lilihitaji kupatiwa dola milioni 445, lakini kupitia taarifa  iliyotolewa na mratibu wa shughuli zake katika kanda hiyo,Mamadou Duian Balde, shirika hilo limesema watu wanaowasili katika eneo la mpakani kutoka Sudan wanajikuta katika hali ngumu kutokana na kukosekana kwa huduma za kutosha, pamoja na miundo mbinu mibovu.

Mpaka sasa shirika hilo limepokea asilimia 19 tu ya dola bilioni 1 wanazohitaji kununua misaada muhimu ya kibinadamu,kama maji,chakula na malazi.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW