1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jenerali AbdelFatah al Burhani wa Sudan yupo ziarani Sudan

4 Septemba 2023

Mkuu wa majeshi nchini Sudan Jenerali Abdel-Fattah Burhani anaelekea Sudan Kusini kwa mazungumzo na rais wa nchi hiyo yatakayojikita katika suala la vita vinavyoendelea nchini Sudan.

https://p.dw.com/p/4Vv2K
Krieg im Sudan | General Abdel Fattah al-Burhan
Mkuu wa jeshi Sudan Abdel Fattah al-Burhan katika picha ya pamoja na raiaPicha: Sudanese Army/AFP

Ziara hiyo ya Burhan ni ya pili nje ya nchi yake tangu vilipozuka vita mwanzoni mwa mwaka huu.

Wiki iliyopita alikwenda Misri alikokutana kwa mazungumzo  na rais Abdel Fattah El Sissi.

Soma pia:Shambulio la anga lawaua raia 20 huko Sudan

Kwa mujibu wa baraza la uongozi la Sudan, Katika ziara yake nchini Sudan Kusini leo hii ameandamana na kaimu waziri wake wa mambo ya nje Ali al-Sadiq pamoja na mkuu wa idara ya Ujasusi,jenerali Ahmed Ibrahim Mufadel.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW