1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

UN: Tuna wasiwasi baada ya China kuwafunga jela wanaharakati

Hawa Bihoga
11 Aprili 2023

Mkuu wa Shirika la Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema ana wasiwasi mkubwa baada ya China kuwahukumu mawakili wawili mashuhuri wa haki za binadamu kifungo cha zaidi ya miaka kumi jela.

https://p.dw.com/p/4PtCr
Schweiz, Genf: Volker Türk, UN-Hochkommissar für Menschenrechte
Picha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/dpa/picture alliance

Xu Zhiyong na mwenzake Ding Jiaxi wote wakiwa ni viongozi wa vuguvugu la kundi la kutetea haki za kiraia lililotaka mageuzi ya katiba na kukosoa ufisadi wa serikali, walipatikana na hatia ya kile kilichotajwa kupindua mamlaka ya serikali katika mashauri yalioendeshwa faraghani.

Turk amesema, wamehukumiwa vifungo virefu,  kinyume na sheria za kimataifa za haki za binadamu na kutaka uchunguzi sahihi katika madai yoyote yanayohusu watetezi wa haki za binadamu.

Xu, ambaye alimtaka Rais Xi Jinping ajiuzulu kutokana na jinsi alivyoshughulikia janga la Corona, alifungwa jela miaka 14, huku Ding akifungwa miaka 12 na kunyimwa haki ya kisiasa kwa miaka 3.