1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Wanaharakati wawili wahukumiwa zaidi wa muongo China

10 Aprili 2023

Wanasheria wawili mashuhuri wa haki za binaadamu nchini China, akiwemo mmoja aliyemtaka kiongozi wa Chinas Xi Jinping ajiuzulu, wamefungwa jela kwa zaidi ya muongo mmoja.

https://p.dw.com/p/4Ps6M
Taiwan Taipeh AI Aktion Bürgerrechtler China
Picha: Wiktor Dabkowski/ZUMA Press Wire/dpa/picture alliance

Habari hizi ni kwa mujibu wa kundi la utetezi wa haki pamoja na mmoja kati ya wake wa wahukumiwa. Kwa mujibu wa kesi iliyokuwa ikiwakabili Xu Zhiyong na mpiga kampeni mwenzake Ding Jiaxi walipatikana na hatia ya kuidharau mamlaka ya serikali.

Wote wawili walikuwa vinara wakuu katika vuguvugu la "New Citizens Movement," kundi la kutetea haki za kiraia lililotaka mageuzi ya katiba na kukosoa ufisadi wa serikali ya China.

Kwa mujibu wa shirika la utetezi wa haki za binaadamu la Human Rights Watch, Xu, ambaye alimtaka Rais Xi ajiuzulu kutokana na jinsi alivyoshughulikia janga la UVIKO-19, alifungwa jela miaka 14, na mwenzake Ding miaka 12.