1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Polisi Bangladesh inamshikilia kiongozi wa upinzani

Hawa Bihoga
29 Oktoba 2023

Polisi nchini Bangladesh imemkamata kiongozi mkuu wa chama cha upinzani wakati kukishuhudiwa maandamano ya kitaifa yakipinga mashambulizi dhidi ya mkutano wake wa kuipinga serikali.

https://p.dw.com/p/4YAIe
Kiongozi wa chama cha upinzani Bangladesch Mirza Fakhrul Islam
Kiongozi wa chama cha upinzani Bangladesch Mirza Fakhrul IslamPicha: Rafayat Haque Khan/Zuma/picture alliance

Msemaji wa chama hicho cha upinzani Shairul Kabir Khan amesema Polisi ilimkamata Katibu Mkuu wa chama cha kizalendo cha Bangladesh Nationalist Party (BNP) Mirza Fakhrul Islam akiwa nyumbani kwake.

Chama hicho cha upinzani Bangladesh kilitangaza kufungwa kwa shughuli zote nchini humo leo Jumapili, baada ya maandamano yaliopangwa kufanyika yakilenga kushinikiza kumuondoa mamlakani waziri mkuu Sheikh Hasina, kuvurugwa na polisi na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo afisa mmoja wa polisi huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Soma pia: Maelfu waandamana Bangladesh kumtaka Waziri Mkuu kujiuzulu

Jeshi la Polisi Bangladesh limesema Mirza alikamatwa kwa mahojiano kuhusu matukio ya siku ya Jumamosi lakini hakina mashataka yoyote yaliotangazwa dhidi yake.