1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN walaani ukatili dhidi ya wafanyakazi wa mashirika

17 Agosti 2023

Umoja wa Mataifa umesema jumla ya wafanyakazi 62 wa mashirika ya misaada wameuawa mnamo mwaka huu duniani kote tangu kufanyika mashambulio makubwa kwenye makao ya Umoja wa Mataifa ya mjini Baghdad, miaka 20 iliyopita.

https://p.dw.com/p/4VI34
Südsudan UN Friedensmission/Symbolbild
Picha: Ashraf Shazly/AFP

Umoja huo unaadhimisha siku ya misaada ya kibinadamu tarehe 19 mwezi Agosti kila mwaka kukumbuka shambulio la kujitoa mhanga lililosababisha vifo vya watu 22 ikiwa pamoja na chaaliyekuwa kamishna wake wa haki za binadamu hayati Sergio Vieira de Mello.

De Mello alikuwa mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq. Pamoja na vifo hivyo vya watumishi wa Umoja wa Mataifa vilivyotukia kwenye maeneo ya mizozo duniani kote, wafanyakazi wengine wa misaada 84 walijeruhiwa na wengine 34 walitekwa nyara.

Soma pia:UN: Yatoa wito wa kupelekwa kikosi cha kimataifa nchini Haiti

Mwaka uliopita watumishi 116 wa umoja huo waliuawa. Sudan imetajwa kuwa mahala pa hatari zaidi kwa wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada.