1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Von der Leyen ataka hatua zaidi kukabili uhamiaji haramu

17 Septemba 2023

Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen ameelezea umuhimu wa kuimarisha hatua za ufuatiliaji kutoka angani na baharini ili kukabiliana na wahamiaji wanaokwenda Ulaya kupitia Bahari ya Mediterania.

https://p.dw.com/p/4WRaq
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen(kushoto) pamoja na waziri mkuu wa Italia, Giorgia Meloni wakati kiongozi huyo wa Ulaya alipokwenda kushuhudia mzozo wa uhamiaji, Lampedusa, Septemba 17,2023.
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen(kushoto) pamoja na waziri mkuu wa Italia, Giorgia Meloni wakati kiongozi huyo wa Ulaya alipokwenda kushuhudia mzozo wa uhamiaji, Lampedusa, Septemba 17,2023.Picha: YARA NARDI/REUTERS

Von der Leyen amesema hayo alipotembelea kisiwa cha Lampedusa nchini Italia kushuhudia mzozo wa wahamiaji, baada ya maelfu ya watu kuingia kisiwani humo hivi karibuni wakitokea kaskazini mwa Afrika, hatua iliyofanya Lampedusa kutangaza hali ya hatari.

Kiongozi huyo aidha ameunga mkono kusakwa kwa njia mpya za kuimarisha operesheni za kijeshi baharini ama kutafutwa kwa mbinu mpya.

Waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni aliyeongozana na Von der Leyen ametoa wito wa kuwazuia wahamiaji kuondoka Afrika, akisema hilo ni jukumu la Umoja wa Ulaya.