1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meloni; Tushirikiane kudhibiti wimbi la wahamiaji Ulaya

24 Julai 2023

Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni ametoa wito wa kuwepo uhusiano kati ya Ulaya na nchi ambako wahamiaji wanatoka na wanakopitia, huku akipendekeza njia kuu nne za ushirikiano wa siku zijazo, kati ya Ulaya na Afrika.

https://p.dw.com/p/4UJ7D
Österreich | 27. Europa-Forum Wachau: Giorgia Meloni
Picha: Alex Halada/IMAGO

Akizungumza jana Jumapili katika Mkutano wa kilele wa Kimataifa wa Maendeleo na Uhamiaji uliofanyika mjini Roma na kuzihusisha takribani nchi 20, Meloni amesema ushirikiano mkubwa unahitajika kati ya mataifa ili kukabilianana wimbi la wahamiaji wanaoingia Ulaya kwa msaada wa Afrika.

Mkutano huo unakusudia kuifanya Italia kuwa kiongozi katika kutatua masuala yanayoathiri mataifa yaliyoko katika Bahari ya Mediterania.

Soma pia:Meloni: Ushirikiano mkubwa unahitajika kukabiliana na wahamiaji wanaoingia Ulaya

Jambo kuu miongoni mwake ni uhamiaji, kwani Italia inawahifadhi mamia ya wahamiaji wapya wanaowasili kila siku kwenye mpaka wa kusini mwa Ulaya, lakini pia nishati, huku Ulaya ikiitazama Afrika na Mashariki ya Kati kama zitakazochukua nafasi ya kudumu ya usambazaji wa Urusi.

Meloni amesema kuna uwezekano kuwa kiburikinachoonyeshwa na mataifa ya Magharibi, kimekuwa kikwazo katika kutafuta suluhisho la suala la uhamiaji.