1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Umoja wa Mataifa wazuru Afghanistan

20 Januari 2023

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed amekutana na naibu gavana wa jimbo la Kandahar nchini Afghanistan katika mkutano usiokuwa wa kawaida kuwahi kufanywa.

https://p.dw.com/p/4MVN0
Äthiopien UN-Untergeneralsekretärin Amina Mohammed in Addis Abeba
Picha: Solomon Muchie/DW

Mkutano huu sio wa kawaida kuwahi kufanywa na mjumbe wa kigeni na viongozi wa Taliban katika eneo la kusini mwa Afghanistan. Mjumbe huyo wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa anayeitembelea Afghanistan katika ziara yake iliyoanza wiki hii alikutana pia na maafisa wengine mjini Kabul pamoja na wafanyakazi wa Umoja huo na mashirika ya msaada  kujadili njia za kuunga mkono na kulinda haki za wanawake. Naibu gavana Maulvi Hayatullah Mubarak  amemwambia mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa kwamba utawala wa Taliban unataka mahusiano mazuru na ulimwengu  na kutowa mwito wa kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya viongozi wa Taliban.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW