1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa watiwa wasiwasi na kutanuka mzozo wa Sudan

27 Juni 2023

Umoja wa Mataifa umesema mzozo wa Sudan unatanuka kuelekea "viwango vya kutia wasiwasi" huko katika jimbo la Darfur na unachukua mkondo wa mgawanyiko wa kikabila.

https://p.dw.com/p/4T8JJ
Sudan Soldaten der RSF Truppe
Picha: Rapid Support Forces/AFP

Darfur, mkoa wa magharibi mwa nchi hiyo kwenye mpaka na taifa la Chad imeshuhudia machafuko ya kutisha tangu kuzuka kwa mapigano kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha wapiganaji wenye nguvu cha RSF mnamo Aprili 15.

Naibu Mkuu wa Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), Raouf Mazou, amesema wanatiwa wasiwasi kutokana na ripoti wanazopokea kutoka mkoa huo juu ya kusambaa kwa machafuko kwa kiwango cha kutisha. 

Soma zaidi: Raia wa Sudan wazidi kuyakimbia mapigano
 

Umoja wa Mataifa wataka mapigano yakomeshwe Darfur

 

Amesema hali hiyo imefanya kuwa vigumu kwa watoa huduma za msaada wa kiutu kuwafikia watu wenye mahitaji.

Mazou pia amezungumzia kurejea kwa migawanyiko ya kikabila iliyougubika mkoa wa Darfur mwanzoni mwa miaka ya 2000. Wakati huo jamii za wachache zililamika kuwa zinatengwa na kunyanyaswa na serikali iliyokuwa ikiongozwa na jamii za Waarabu.