1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wataka mapigano yakomeshwe Darfur

24 Juni 2023

Umoja wa mataifa hii leo umetaka hatua za haraka zichukuliwe ili kukomesha mauaji ya raia wasio na hatia wanaoukimbia mji mkuu wa jimbo la Darfur Magharibi wa El-Geneina.

https://p.dw.com/p/4T1EF
Sudan | Sicherheitskräfte
Picha: Ashraf Shazly/AFP/Getty Images

Makundi ya watu wenye silaha na wanaoungwa mkono na wanajeshi wa dharura wa RSF wanasababisha mauaji hayo. Kwa zaidi ya miezi miwili, jeshi la Sudan, likiongozwa na Jenerali Abdel Fattah -al Burhan limekuwa kwenye mapambano dhidi ya wanajeshi wa RSF wanaomtii aliyekuwa msaidizi wake Mohamed Hamdan Daglo.

Soma zaidi: Miji ya Darfur yashambuliwa huku vita vya Sudan vikisambaa

Kutokana na machafuko kwenye jimbo la Darfur, Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa mzozo huo umechukua sura mpya ya mapigano ya kikabila. Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa inayoshughulika na haki za binadamu imesema kuwa watu wanaokimbilia nchi jirani ya Chad wakitembea kutoka Darfurwameelezea juu ya kuwepo kwa matukio ya kutisha yanayofanywa na wabeba silaha wenye asili ya kiarabu wanaoungwa mkono na jeshi la dharura la RSF.