1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wataka kusimamishwa mapigano Sudan Kusini

16 Machi 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito wa kukomeshwa haraka mapigano Sudan Kusini. Baraza hilo pia limeitaka serikali ya nchi hiyo ihakikishe uchaguzi uliocheleweshwa unafanyika kwa amani mwaka ujao.

https://p.dw.com/p/4OlHG
Sudan | Papst Franziskus in Juba
Picha: Vatican Media/abaca/picture alliance

Wanachama 13 wa baraza hilo wameunga mkono azimio hilo wakati China na Urusi hazikupiga kura. Umoja wa Mataifa pia umeongeza muda wa jukumu la kulinda amani linalotekelezwa na askari wake nchini Sudan Kusini.

Askari hao 17,000 wa Umoja wa Mataifa wataendelea na jukumu hilo hadi mwezi Machi mwaka ujao.

Rais wa Sudan Kusini atoa wito kwa wakimbizi kurejea nyumbani

Wakati huo huo, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini Nicholas Haysom ameelezea matumaini kwamba nchi hiyo itaweza tu kutekeleza ahadi ya kuandaa uchaguzi mwaka ujao endapo patakuwapo dhamira ya kisiasa.