1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa waomba msaada wa dola milioni 18.5 kwa Mpox

21 Agosti 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la Wahamiaji, IOM, limeomba msaada wa dola milioni 18.5 kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa watu walioathiriwa na mripuko wa homa ya Mpox Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

https://p.dw.com/p/4jj8L
Mchoro wa Mpox unaonyesha mirija ya majaribio yenye lebo chanya ya virusi vya Mpox
Vipimo vya Mpox vinaonyesha mirija ya majaribio yenye lebo ya virusi vya Mpox Agosti 20, 2024.Picha: Dado Ruvic/Illustration/REUTERS

Mkurugenzi Mkuu wa IOM, Amy Pope amesema kusambaa kwa visa vya Mpox katika eneo la Mashariki, Pembe na Kusini mwa Afrika, ni jambo linaloleta wasiwasi mkubwa. Pope amesema wasiwasi mkubwa uko hasa kwa wahamiaji wanaoishi katika mazingira magumu, watu wanaohama sana na jamii zilizohamishwa ambazo mara nyingi hazizingatiwi katika majanga kama hayo.Wakati huo huo, Thailand imesema imegundua kisa cha homa ya mpox kwa mwanaume mmojawa Ulaya ambaye ameingia nchini humo akitokea Afrika. Idara ya Kudhibiti Magonjwa imesema leo kuwa mwanaume huyo anasubiri majibu ya vipimo ili kubaini kama ni aina aina mpya ya kirusi cha Mpox Clade 1b.