1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yakubali kuisaidia Kongo kusafirishaji vifaa vya kura

16 Desemba 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeruhusu ujumbe wa kulinda amani wa Umoja huo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO kutoa msaada wa usafirishaji wa vifaa vya kura kwa ajili ya uchaguzi wa wiki ijayo

https://p.dw.com/p/4aF1F
Mwanajeshi wa kikosi cha MONUSCO karibu na Kibumba. Kaskazini mwa Goma nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, mnamo Januari 28, 2022
Mwanajeshi wa kikosi cha MONUSCO nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya KongoPicha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Barua kutoka kwa rais wa baraza hilo la usalama, imesema kwamba kwa kuzingatia umuhimu wa kuanza kwa haraka kuandaa msaada ambao Kongo imeomba, wanachama wa baraza hilo wanapanga kumfahamisha katibu mkuu wa Umoja huo kwamba kikosi hicho cha MONUSCO kimepewa idhini ya kutoa msaada huo kwa ajili ya mchakato wa uchaguzi kama ilivyoomba na serikali ya Kongo.

Soma pia:Kikosi cha Afrika Mashariki chaanza kuondoka Kongo

Barua hiyo imeendelea kueleza kuwa msaada huo wa MONUSCO utatolewa kwa kiwango ambacho hakitaathiri uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya awali. Serikali ya Kongo imetaka kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa kuondoka nchini humo baada ya kuhudumu kwa takriban miaka 20, na kusema kuwa kimeshindwa kumaliza mapigano nchini humo.