1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wahitaji dola bilioni 3 kwa ajili ya Sudan

17 Mei 2023

Umoja wa Mataifa umesema leo kuwa takribani dola bilioni tatu za Kimarekani zitahitajika ili kutoa misaada ya dharura kwa watu walioathiriwa na mapigano nchini Sudan.

https://p.dw.com/p/4RURk
Sudan Khartum Kämpfe Bürgerkrieg
Picha: Mohamed Nureldin/REUTERS

Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu wa Shirika la Misaada yaKkiutu la Umoja wa Mataifa, Ramesh Rajasingham, amesema msaada huo pia utawasaidia zaidi ya watu milioni moja wanaotarajiwa kukimbilia nchi za karibu mwaka huu. 

"Mahitaji nchini Sudan ni muhimu na yapo kila mahali kama unavyoweza kutarajia kutoka kwenye mapigano. Kunahitajika msaada wa kimatibabu, chakula, usafi, makaazi na mshtuko. Na pia tunapokea ripoti zenye kutia wasiwasi za ongezeko la udhalilishaji wa kingono huku wahanga wakiwa bila msaada." Alisema.

Soma zaidi: Sudan yageuka uwanja wa mapigano kwa wapiganaji wa kigeni

Mapigano nchini Sudan yamezidisha mzozo wa kiutu nchini humo ambapo kati ya dkila watu watatu, mmoja alikuwa anategemea misaada hata kabla mapigano.

Madaktari wanasema karibu watu elfu moja wamefariki dunia ndani na nje ya Khartoum pamoja na jimbo la Darfur.