1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa waahidi kubakia Afghanistan

6 Mei 2023

Umoja wa Mataifa umethibitisha tena ahadi yake ya kubakia Afghanistan, hii ni kulingana na mapitio ya tathmini ya operesheni zake nchini humo, licha ya Taliban kuwazuia wanawake kufanya kazi kwenye mashirika ya umoja huo

https://p.dw.com/p/4QygX
USA New York | UN-Vollversammlung | Antonio Guterres
Picha: Mary Altaffer/AP Photo/picture alliance

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Farhan Haq amewaambia waandishi wa habari kwamba ujumbe wa umoja huo nchini Afghanistan UNAMA, umeahidi kubakia nchini humo kwa niaba ya wanaume, wanawake na watoto wa Afghanistan.

Soma zaidi:Mataifa yajadili haki za wanawake wa Afghanistan

Umoja huo ulizindua tathmini iliyoangazia ikiwa itaendelea kufanya kazi na Taliban na hasa baada ya zuio hilo na hatimaye jana kutoa tamko hilo.

Katika taarifa iliyotolewa mjini Kabul, UNAMA ilirudia tena kulaani marufuku hiyo, ambayo imesema inadhoofisha majukumu yao na uwezo wa kufikia watu wote na kuahidi kuendelea kujadiliana na serikali namna watakavyoshirikiana.