1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa kuunda tume huru kuchunguza shambulio la kigaidi katika ofisi zake za Algeria

15 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CphO

NEW YORK:

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa-Ban Ki-moon amesema kuwa atateua tume huru kufanya uchunguzi wa shambulio la kigaidi ambalo liliwauwa wafanya kazi 17 wa umoja wa Mataifa mjini Algiers Algeria mwezi jana.Tume huru itakuwa na wataalamu wakimataifa kutoka nje ya mfumo wa Umoja wa Mataifa na itaomba ushirikiano wa karibu na wakuu wa Algeria.Shambulio la kujitoa mhanga la Disemba 11 liliuwa watu wasiopungua 41 mkiwemo watumishi 17 wa Umoja wa Mataifa.Tawi la Algeria la kundi la kigaidi la mtandao wa Al-Qaida ndio lilidai kuhusika.