1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Ulaya na Marekani zasusia kutoa heshima kwa Raisi

31 Mei 2024

Kikao maalumu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kutoa heshima kwa rais wa Iran aliyefariki dunia Ebrahim Raisi, kilipuuzwa jana na mataifa ya Ulaya magharibi na mashariki huku kukiwa na upinzani dhidi ya hatua hiyo

https://p.dw.com/p/4gTMu
Raia wa Iran mjini Mashhad watoa heshima zao za mwisho kwa Rais Ebrahim Raisi na wenzake waliofariki kwenye ajali ya helikopta, Mei 23,2024
Raia wa Iran watoa heshima zao za mwisho kwa Rais Ebrahim Raisi Picha: Iranian Presidency Office/AP/picture alliance

Kikao hicho cha kutoa heshima ni utaratibu wa muda mrefu ambapo Baraza hilo la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 193 hufanya mkutano maalumu kwa heshima ya kumbukumbu ya mkuu wa nchi mwanachama anapofariki.

Soma pia:Rais Assad wa Syria akutana na kiongozi Mkuu wa Iran Khamenei

Makundi yote ya kikanda ya Umoja wa Mataifa hutuma wawakilishi kuzungumza juu ya maisha ya mwendazake na urithi alioacha.

Rais Raisi alikumbukwa kwa sifa kemkem hasa kutoka mataifa ya Afrika.

Soma pia:Mamilioni ya waombolezaji wajitokeza kutoa heshima zao kwa Rais Ebrahim Raisi

Lakini kilichotokea jana ambacho hakikuwa cha kawaida ni kwamba ni wawakilishi kutoka Afrika, eneo la Asia-Pasifiki na Amerika ya Kusini tu pamoja na makundi ya kikanda ya eneo la Karibia waliozungumza.

Ulaya na Marekani zasusia kutoa heshima kwa Raisi

Hakukuwa na hotuba kutoka kwa mataifa ya Ulaya magharibi na mashariki, ama pia Marekani, ambayo kwa kawaida huzungumza ya mwisho ikiwakilisha nchi mwenyeji.