1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Rais Assad wa Syria akutana na Kiongozi Mkuu Iran Khamenei

30 Mei 2024

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amemkaribisha Rais Bashar al-Assad wa Syria mjini Tehran leo aliyesafiri kwenda nchini humo kutoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Rais wa Iran Ebrahim Raisi.

https://p.dw.com/p/4gT1k
Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei
Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali KhameneiPicha: Atta Kenare/AFP

Ikulu ya Syria imesema katika mazungumzo ya viongozi hao wawili yaliyohudhuriwa pia na rais wa mpito wa Iran Mohammad Mokhber, Assad na Khamenei wamesisitiza kwamba usuhuba kati ya nchi hizo washirika bado ni madhubuti. 

Kwa zaidi ya muongo mmoja sasa Iran imesalia kuwa muungaji mkono pekee wa utawala wa Assad ulionusurika kuangushwa wakati wa wimbi la mapinduzi ya umma katika ulimwengu wa kiarabu mwanzoni mwa miaka ya 2010.

Soma pia:Iran yasema Saudi Arabia imewafukuza waandishi habari 6 wa televisheni ya taifa ya Iran

Safari ya Assad mjini Tehran imefanyika katika siku ambayo mamlaka za Iran zimefungua pazia la usajili wagombea wanaotaka kuwania nafasi ya Urais kurithi ile iliyoachwa na hayati Ebrahim Raisi. Usajili utafanyika kwa siku tano na kufuatia na zoezi la mchujo wagombea kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Juni 28.