1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yasema inaimarisha nafasi ya vikosi vyake, Urusi

17 Agosti 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema leo kwamba vikosi vyake vinajiimarisha katika eneo la Kursk nchini Urusi, ambako Ukraine imekuwa ikiendeleza mashambulizi makubwa ya ardhini kwa zaidi ya siku 11.

https://p.dw.com/p/4ja7v
Gari la kijeshi la Ukraine lapita eneo la mpaka wake na Urusi lililoharibiwa katika eneo la Sumy mnamo Agosti 14,2024
Gari la kijeshi la Ukraine lapita eneo la mpaka wake na Urusi lililoharibiwaPicha: ROMAN PILIPEY/AFP

Matamshi ya Rais Zelensky yanakuja siku moja baada ya Urusi kuishutumu Ukraine kwa kuharibu daraja muhimu  katika eneo hilo la mpakani, huku Ukraine ikitafuta kuvuruga njia za usambazaji bidhaa na zinazotumiwa na wanajeshi wa Urusi katika eneo hilo.

Soma pia:Ukraine, Urusi zadai kuimarisha mashambulizi

Katika taarifa kupitia mtandao wa Telegram, Rais Zelensky amesema kuwa mkuu wa jeshi lake Oleksandr Syrsky ameripoti kuhusu uimarishaji wa nafasi ya vikosi vya nchi hiyo katika mkoa wa Kursk .

Urusi yasema imevirudisha nyuma vikosi vya Ukraine

Wizara ya ulinzi ya Urusi, imesema leo kuwa imevirudisha nyuma vikosi vya Ukraine karibu na maeneo matatu ya makazi katika eneo laKurskna linayasaka makundi ya adui yanayojaribu kupenya zaidi kwenye ardhi ya nchi hiyo.