1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine: Uvamizi Kursk walenga "mazungumzo ya haki"

16 Agosti 2024

Ukraine imesema leo kuwa uvamizi wake ndani ya ardhi ya Urusi unalenga kuilazimisha Moscow kurudi katika meza ya majadiliano kwa "masharti ya haki."

https://p.dw.com/p/4jYvF
Russland | Die Lage in der Region Kursk nach dem Beschuss der ukrainischen Streitkräfte
Picha: Anatoliy Zhdanov/Kommersant/Sipa USA/picture alliance

Msaidizi wa Rais Volodymyr Zelensky, Mykhailo Podolyak, amesema nchi hiyo inataka kujadiliana na Urusi kwa masharti yao wenyewe.

Mykhailo ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba, hawana mpango wa kunyenyekea wakati wa majadiliano na Urusi.

Mapema wiki hii, vikosi vya Ukraine vilipiga hatua kubwa katika vita vyake na Urusi kwa kuchukua udhibiti wa mji mdogo wa Sudzha uliopo kwenye mkoa wa mpakani wa Urusi wa Kursk.

Ukraine hata hivyo imeondoa uwezakano wa kufanya mazungumzo na Urusi iwapo vikosi vya Moscow havitaondoka katika ardhi ya Ukraine.