1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Baerbock, azuru Kyiv

11 Septemba 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock, anafanya ziara nchini Ukraine leo kwa dhima ya kuendelea kuonesha mshikamano na taifa hilo linalopigana vita na Urusi.

https://p.dw.com/p/4WBlK
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock(kulia) akiwasili Kyiv kwa usafiri wa treni kwa ajili ya ziara yake nchini Ukraine.
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock(kulia) akiwasili Kyiv kwa usafiri wa treni kwa ajili ya ziara yake nchini Ukraine.Picha: Oliver Weiken/dpa/picture alliance

Annalena Baerbock aliwasili mjini Kyiv mapema asubuhi akitumia usafiri wa treni kutokea Poland na amepangiwa kuwa na mazungumzo na viongozi wakuu wa Ukraine.

Katika taarifa aliyoitoa akiwa njiani kuelekea mjini Kyiv, Baerbock amesema Ujerumani itaendelea kuisadia Ukraine kijeshi, kiuchumi na kiutu katika mapambano yake ya kuishinda Urusi.

Mwanadiplomasia huyo pia amearifu ziara hiyo ya leo ambayo ni ya nne tangu Urusi ilipoivamia Ukraine, inalenga kutathimini hatua zilizopigwa kuelekea azma ya taifa hilo kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Amesema serikali mjini Berlin iko tayari kuisaidia nchi hiyo kuimarisha utawala bora, kupambana na rushwa na kufikia viwango vingine vinavyohitajika kabla ya kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.