1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin anapswa kuwajibishwa kwa uhalifu wa kivita

18 Julai 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ametaka Rais wa Urusi Vladimir Putin awajibishwe kwa uhalifu kutokana na vita alivyovianzisha nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4U2Zo
Kongamano la kuijenga upya Ukraine lililoandaliwa mjini London
Annalena Baerbock - Waziri wa mambo ya nje wa UjerumaniPicha: Henry Nicholls/PA Wire/picture alliance

Akizungumza mjini New York wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya sheria ya Roma iliyopelekea kuanzishwa kwa mahakama ya ICC, Baerbock amesema rais Putin amewasukuma watoto katika vita vyake vya maangamizi.

Baerbock atoa wito wa watoto kurudishwa kwa wazazi wao

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani amemtuhumu Putin kwa kuwateka nyara watoto na kuwanyima utambulisho, ili iwe vigumu kwa wazazi wao kuwatambua na kuwarudisha nyumbani. Ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuhakikisha kwamba watoto hao wanarudishwa kwa wazazi wao.