1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yaipiga meli ya Urusi kwenye rasi ya Crimea

26 Desemba 2023

Jeshi la anga la Ukraine limesema kwamba limeipiga na kuiharibu meli ya Urusi kwenye rasi ya Crimea.

https://p.dw.com/p/4aa7u
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa mkutano wa Jukwaa la Crimea huko Kyiv.Picha: via REUTERS

Ukraine inatuhumu kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba ndege zisizo na rubani kwa ajili ya matumizi ya vita vya Urusi nchini Kyiv.

Soma pia: Zelensky awasifu wanajeshi wake kwa kudungua ndege za Urusi

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Telegram jeshi la Ukraine limeishambulia meli hiyo kwa kutumia makombora katika eneo la Feodosia kwenye Bahari Nyeusi .

Soma pia: Ukraine yasherehekea Krismasi ya kwanza ya Disemba 25

Baada ya shambulizi hilo, Gavana aliyechaguliwa na Moscow, Sergei Aksyonov ameeleza kwamba mtu mmoja ameuwawa na watu wengine wawili wamejeruhiwa. Vile vile nyumba sita zimeharibiwa kwenye kadhia hiyo.