1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUkraine

Ukraine yasherehekea Krismasi ya kwanza ya Disemba 25

25 Desemba 2023

Wakristo wa madhehebu ya Orthodox nchini Ukraine wanasherehekea kwa mara ya kwanza sikukuu ya Krismasi ya Disemba 25 baada ya serikali ya nchi hiyo kubadili tarehe katika juhudi za kujitenga na Urusi.

https://p.dw.com/p/4aY94
Sherehe za kwanza za Krismasi ya Disemba 25 nchini Ukraine
Sherehe za kwanza za Krismasi ya Disemba 25 nchini Ukraine Picha: Evgeniy Maloletka/AP/picture alliance

Kihistoria Ukraine kama ilivyo kwa mataifa mengine mashariki yenye idadi kuwa ya waumini wa Orthodox, imekuwa ikisherehekea Krismasi mnamo Januari 7 kwa kuzingatia kalenda ya Julian.

Hata hivyo Julai mwaka huu rais Volodomyr Zelensky alitia saini sheria inayoamuru Krismasi kusherehekewa Disemba 25 akisema hatua hiyo inatoa nafasi kwa Ukraine kujitenga na urithi wa Kirusi wa kusherehekea sikukuu hiyo tarehe 7 Januari.

Mabadiliko hayo ya tarehe ni sehemu ya hatua pana zinazochukuliwa na taifa hilo kuondoa kumbukumbu zote za mafungamano na Urusi ambayo iliivamia Ukraine kijeshi mwaka jana.

Ukraine ilikuwa sehemu ya kanisa la Orthodox la Urusi lakini ilijitenga baada ya Moscow kuinyakua rasi ya Crimea mnamo mwaka 2014.