1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yadunguwa makombora 14 ya Urusi

8 Desemba 2023

Vikosi vya ulinzi wa anga vya Ukraine vimesema vimeyadungua makombora 14 kati ya 19 yaliyorushwa na Urusi wakati wa shambulizi lake la anga mapema leo asubuhi.

https://p.dw.com/p/4ZwZl
Mwanajeshi wa Ukraine akiwa kwenye uwanja wa mapambano katika mkoa wa Kharkiv.
Mwanajeshi wa Ukraine akiwa kwenye uwanja wa mapambano katika mkoa wa Kharkiv.Picha: Ozge Elif Kizil/AA/picture alliance

Msemaji wa jeshi la anga la Ukraine, Yuryi Ihnat, amesema makombora hayo yalidunguliwa kwenye jimbo lililopo nje ya mji wa Kiev na jimbo la kati la Dnipropetrovsk.

Wakati huo huo, mtu mmoja amejeruhiwa baada ya makombora kadhaa ya Urusi kuushambulia mji wa Kharkiv, mashariki ya Ukraine.

Maafisa wa Ukraine wamesema makombora hayo pia yameharibu majengo ya makaazi.

Soma zaidi: Ukraine yaonya kuwa Urusi inajaribu kuuteka tena mji wa Kupyansk

Mkuu wa utawala wa kijeshi la Kharkiv, Oleg Synegubov, ameandika katika mtandao wa Telegram kuwa mtu mmoja amejeruhiwa na wilaya za Kholodnohirskyi na Shevchenkivskyi zilishambuliwa kwa makombora hayo.

Meya wa Kharkiv, Igor Terekhov, amesema wamehesabu takribani makombora matano.