1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yaonya kuwa Urusi inajaribu kuuteka mji wa Kupyansk

26 Novemba 2023

Jeshi la Ukraine limeonya kuhusu hatari ya Urusi kujaribu tena kuliteka eneo la Kupyansk katika mkoa wa Kharkiv nchini Ukraine, huku vikosi vya Urusi vikiendeleza mashambulizi yake Mashariki mwa nchi hiyo

https://p.dw.com/p/4ZSXX
Wafanyakazi wa msaada watafuta manusura katika vifusi vya majengo yalioporomoka kutokana na shambulizi la Urusi lililosababisha vifo vya watu 47 katika kijiji cha Hroza karibu na Kharkiv mnamo Oktoba 5, 2023
Wafanyakazi wa msaada watafuta manusura katika vifusi vya majengo yalioporomoka kutokana na shambulizi la UrusiPicha: Ukrainian Presidential Press Office/AP Photo/picture alliance

Katika taarifa kupitia televisheni hii leo, msemaji wa jeshi la Ukraine Volodymyr Fityo, amesema wavamizi wa Urusi hawajafutilia mbali nia yao ya kuushambulia mji wa Kupyansk na kwamba wanataka kuukalia tena.

Vikosi vya Urusi vimeendeleza mashambulizi yao Kaskazini Mashariki mwa Ukraine katika wiki za hivi karibuni na kufanikiwa kuyadhibiti maeneo kadhaa.

Soma pia: Urusi yafanya mashambulizi makubwa mjini Kyiv

Mapigano sasa yanafanyika katika kijiji cha Synkivka, kilichoko kilomita chache Kaskazini Mashariki mwa Kupyansk.

Urusi ilifanya uvamizi kamili nchini Ukraine mnamo mwezi Februari mwaka 2022. Katika msimu wa vuli uliopita, Ukraine ilifanikiwa kukomboa sehemu kubwa ya eneo la Kharkiv ikiwa ni pamoja na makutano muhimu ya reli ya Kupyansk katika mto Oskil kama sehemu yake ya mashambulizi ya kulipiza kisasi.