1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yadungua droni na makombora yaliyorushwa na Urusi

23 Oktoba 2023

Ukraine inasema imezidungua droni 14 za mashambulizi pamoja na makombora yaliyorushwa na Urusi kuelekea kusini na mashariki mwa taifa hilo usiku wa kuamkia leo.

https://p.dw.com/p/4XtwJ
Watu wakiangalia gari la kijeshi la Urusi lililoharibiwa na vikosi vya Ukraine
Watu wakiangalia gari la kijeshi la Urusi lililoharibiwa na vikosi vya UkrainePicha: Roman Pilipey/AFP/Getty Images

Hata hivyo, kulingana na maafisa wa Kyiv, mabaki ya droni hizo yaliharibu ghala moja katika bandari ya Bahari Nyeusi kwenye mji wa Odesa.

Gavana wa Odesa, Oleh Kiper, amesema mifumo ya anga iliangusha droni 9 zilizotengenezwa Iran, lakini hakukuripotiwa majeruhi.

Soma pia:Urusi yauwa 6, yajeruhi 16 kaskazini mashariki mwa Ukraine

Aidha Wizara ya mambo ya ndani imesema mashambulizi hayo pia yalilenga mikoa ya Kherson kusini na mashariki mwa Donesk na kaskazini mashariki mwa Sumy.

Urusi ambayo inakana kuwalenga raia, haijasema chochote juu ya shambulizi hilo.