1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yauwa 6, yajeruhi 16 kaskazini mashariki mwa Ukraine

22 Oktoba 2023

Maafisa nchini Ukraine wamesema makombora yaliyorushwa na Urusi kaskazini mashariki mwa eneo la Kharkiv yalililenga jengo la posta na kusababisha mauaji ya wafanyakazi wake sita na kuwajeruhi wengine 16.

https://p.dw.com/p/4Xryb
Mji wa Kharkiv baada ya mashambulizi ya Urusi kwenye mji huo wa kaskazini mashariki ya Ukraine.
Mji wa Kharkiv baada ya mashambulizi ya Urusi kwenye mji huo wa kaskazini mashariki ya Ukraine.Picha: Sofiia Gatilova/REUTERS

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine alichapisha vidio katika mitandao ya kijamii iliyolionesha eneo hilo likiwa limeharibiwa vibaya, huku kukiwa na kontena iliyokuwa na nembo ya kampuni hiyo ya Nova Posta. 

Gavana wa Kharkiv, Oleg Sinegubov, amesema waliojeruhiwa walikuwa kati ya umri wa miaka 19 hadi 42.

Soma zaidi: Urusi: Kupelekwa makombora ya kisasa Ukraine ni tishio

Gavana huyo aliongeza kuwa watu saba kati ya 16 wanaotibiwa hospitalini wako katika hali mahututi. 

Kulingana na waendesha mashitaka wa eneo hilo, wanajeshi wa Urusi katika eneo la Belgorod kaskazini mwa Kharkiv walirusha makombora aina ya S-300 na mawili kati ya makombora hayo yakalenga eneo hilo la posta.