1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yadai kudungua droni 22 za Urusi

5 Juni 2024

Jeshi la anga la Ukraine limedai kuzidungua droni 22 kati ya 27 aina ya Shaheed zilizorushwa kwenye maeneo matano ya Ukraine katika shambulizi la usiku kucha kuamkia leo Jumatano.

https://p.dw.com/p/4gfDB
Videostill | Drone Warfare in Ukraine
Vita vya kutumia ndege zinazorushwa bila ya rubani Drone huko Ukraine.Picha: Max Zander/DW

Shambulizi hilo liliharibu kiwanda kimoja na kumjeruhi mtu mmoja katika mkoa wa Poltava. Haya yameelezwa na gavana wa eneo hilo Filip Pronin, katika ujumbe aliochapisha kwenye mtandao wa Telegram. Gavana wa Mykolaiv amesema jeshi la nchi hiyo liliharibu droni sita katika eneo la kusini la mkoa huo huku mabaki ya droni moja yakiharibu nyumba kadhaa lakini hakuna majeruhi walioripotiwa. Droni nne zilidunguliwa katika eneo la kusini la Kherson na nne nyingine katika mkoa wa kati wa Dnipropetrovsk. Shambulizi hilo pia lililenga eneo la kaskazini la Sumy, lakini hakuna maelezo ya uharibifu ulioripotiwa na mamlaka za huko.