1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi na Ukraine zabadilishana wafungwa

4 Januari 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema Urusi imewachilia huru watu 200, ikiwa ni pamoja na wanajeshi wa vikosi mbalimbali.

https://p.dw.com/p/4aqSX
Rais Volodymyr Zelensky akimkaribisha kamanda Denys Prokopenko
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine akipeana mkono na makamanda wa waliokuwa wakikipigania kiwanda cha chuma cha Azovstal, waliporejea Ukraine kutokea Istanbul, Uturuki Julai 8, 2023Picha: Ukrainian Presidential Press Service/REUTERS

Kulingana na Zelenskyy, watu walioachiliwa huru ni pamoja na wanajeshi walioupigania mji wa Mariupol na kiwanda cha chuma cha Azovstal kilichopo kusini mwa Ukraine.

Zelenskyy amethibitisha hayo kupitia mtandao wa X.

Urusi kwa upande wake ilitangaza Ukraine kuwaachilia huru wanajeshi wake 248, baada ya mazungumzo magumu yaliyosimamiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Falme za Kiarabu imethibitisha jukumu lake hilo, na kusema mabadilishano hayo yamefikiwa kutokana na uhusiano wa karibu kati yake na Urusi na Ukraine na kuahidi kuendeleza juhudi za kupatikana suluhu.