1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Ukraine wahamishwa kutoka Mariupol

17 Mei 2022

Mamia ya wanajeshi wa Ukraine wamehamishwa kutoka kiwanda kikubwa cha chuma cha Azovstal - ambayo yalikuwa maficho ya mwisho ya wanajeshi waliokuwa wanaulinda mji wa bandari ya kusini wa Mariupol.

https://p.dw.com/p/4BO8f
Ukraine Nowoasowsk | Ankunft Busse mit Ukrainischen Soldaten aus dem Stahlwerk Asowstal
Picha: Alexander Ermochenko/REUTERS

Naibu waziri wa ulinzi wa Ukraine Ganna Malyar amesema zaidi ya askari 260 wamehamishwa kupitia maeneo yaliyowekwa ya kiutu hadi maeneo yaliyo chini ya Moscow na udhibiti wa wanaharakati wanaopigania kujitenga wakiungwa mkono na Urusi. Malyar amesema utaratibu wa kubadilishana askari utafanywa ili warejee nyumbani.

Jeshi la Ukraine limesema wanajeshi waliokuwa mjini Mariupol walifanya kazi yao ya mapigano na sasa lengo kubwa ni kuyaokoa maisha ya askari.

Taarifa ya jeshi imesema kwa kukishikilia kiwanda hicho cha chuma, waliwazuia wanajeshi wa Urusi kuukamata kwa kasi mji wa kusini wa Zaporizhzhia. Licha ya raslimali ilizo nazo jirani yake, Ukraine imemudu kulirudisha nyuma jeshi la Urusi kwa kipindi kirefu kuliko ilivyotarajiwa na wengi, ikisaidiwa na silaha na fedha kutoka kwa washirika wa Magharibi.

Mengi zaidi yatafuata.......