1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine inasema Urusi inapelekea wanajeshi wachache Avdiivka

22 Novemba 2023

Maafisa wa Ukraine wamesema kuwa Urusi inaonekana kutuma wanajeshi wachache na silaha katika uwanja wa mapambano kwenye mji ulioharibiwa kwa vita wa Avdiivka.

https://p.dw.com/p/4ZHuq
Athari ya vita katika mji wa Avdiivka
Uharibifu wa majengo uliosababishwa na mashambulizi ya vikosi vya Urusi katika mji wa AvdiivkaPicha: Radio Free Europe/Radio Liberty/Serhii Nuzhnenko via REUTERS

Maafisa wa Ukraine wamesema kuwa Urusi inaonekana kutuma wanajeshi wachache na silaha katika uwanja wa mapambano kwenye mji ulioharibiwa kwa vita wa Avdiivka, ambao unachukuliwa kama mlango wa kuingia katika mji mkuu wa mkoa wa Donetsk.

Msemaji wa jeshi la Ukraine Oleksandr Shtupun ameeleza kuwepo kwa mashambulizi madogo ya ardhini na angani huko Avdiivka, mji uliokuwa na idadi ya watu 32,000 kabla ya vita hivyo kuanza.

Takriban wakaazi 1,500 tu ndio waliosalia. Mji huo ulikabiliwa na mashambulizi ya Urusi kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Urusi inaonekana kutoutaja mji wa Avdiivka katika ripoti zake za oparesheni za kijeshi za kila siku. Taarifa ya hivi karibuni ya jeshi la Urusi imeeleza kuwa, askari wake wanafanya mashambulizi katika vijiji vya kusini mwa Avdiivka japo walitoa maelezo kidogo tu.

Shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha ripoti zilizotolewa na pande zote mbili kwenye vita hivyo.