1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi imesema haiweza kwenda sambamba na utawala wa Ukraine.

21 Novemba 2023

Urusi imesema haiwezi kuishi pamoja na utawala wa sasa wa Ukraine na kwamba itaendelea kukabiliana na shinikizo la Jumuiya ya Kujihami NATO kwa muda utakaohitajika hadi kufikia malengo yake.

https://p.dw.com/p/4ZGXv
Südafrika | BRICS Wladimir Putin
Picha: Sergei Bobylev/dpa/picture alliance

Hayo ni kulingana na kauli iliyotolewa leo mjini Moscow na mwanadiplomasia mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Balozi Rodion Miroshnik, ambaye amesema Ukraine imefanya uhalifu dhidi ya raia na kwamba NATO iliipatia silaha zilizopigwa marufuku, huku akisisitiza kuwa ipo siku mataifa ya Magharibi yataitelekeza Ukraine.Hayo yakijiri, washirika wakuu wa Ukraine katika uvamizi huu wa Urusi ambao ni Marekani na Ulaya, wamesisitiza uungaji mkono usiotetereka kwa Kyiv. Jana na leo, mawaziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na yule wa Ujerumani Boris Pistorius wamefanya ziara za kushtukiza mjini Kiev ili kuthibitisha msimamo huo.Wakati huo huo, Ofisi ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa imesema zaidi ya raia 10,000 wameuawa nchini Ukraine tangu Urusi ilipoivamia Februari mwaka jana.