Ujerumani yavizima vinu vya mwisho vya nishati ya nyuklia
15 Aprili 2023Vinu vitatu vya mwisho vya nishati ya atomiki nchini Ujerumani vinazimwa leo Jumamosi, na Ujerumani haitotengeneza tena kawi ya nyuklia siku za usoni.
Kuzimwa kwa vinu hivyo vya Isar 2 jimboni Bavaria, Neckarwestheim 2 jimboni Baden-Wuertemberg na Emsland cha jimboni Lower Saxony, ukurasa wa enzi ya nishati ya nyuklia umefungwa nchini Ujerumani, miongo sita baada ya kufunguliwa.
Mchakato wa kuachana na nishati ya nyuklia nchini Ujerumani ulianzishwa na kansela wa zamani Angela Merkel, kufuatia ajali katika kinu cha nyuklia cha Fukushima nchini Japan mwaka 2011.
Wakati huo ilitarajiwa kuwa kinu cha mwisho nchini Ujerumani kingezimwa mwisho mwishoni mwa mwaka 2022, lakini muda huo ulisogezwa mbele na kansela wa sasa Olaf Scholz kutokana kutokana na mgogoro wa nishati uliofuatia uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.
Vyanzo: dpa, epd